
Ni mwezi mmoja tu umebaki hadi kufikia mwezi January ambapo dirisha dogo la usajili barani Ulaya litafunguliwa rasmi, bado dirisha la usajili halijafunguliwa lakini headlines za mchezaji gani atajiunga na timu gani mwezi January zina zidi kuchukua nafasi.
Kocha wa Man United Jose Mourinho ameanza kuhusishwa kuwa katika mpango wa kumsajili Willian wa Chelsea mwezi January, stori kutoka dailystar na 101greatgoals.com imeeleza kuwa Mourinho anataka kumsajili Willian ambaye imeanza kuaminika kuwa anakosa nafasi chini ya Antonio Conte.

Willian akiwa na kocha Jose Mourinho wakati wakiwa pamoja Chelsea