- 7 Januari 2017
Genge moja la uhalifu linaloendesha shughuli zake katika magereza mbalimbali nchini Brazil, limewakata vichwa takriban wafungwa 33 katika gereza moja katika jimbo la Kaskazini la Roraima.
Ni tukio la pili chini ya juma moja kutokea nchini Brazil.
Maafisa wa Serikali wanaamini kuwa kukatwa vichwa huko kunatokana na mzozano unaondelea miongoni mwa wanachama wa genge hilo lijulikanalo kama PCC.
Gereza hilo lililosongamana liko eneo la mashambani, nje ya mji mkuu wa jimbo wa Boa Vista.
Hadi kufikia sasa maiti 31 zimepatikana. nyingi ya maiti hizo zimekatwa vichwa au kukatwakatwa vipande.
Maafisa wa Serikali wanasema ghasia hizo ni sehemu ya juhudi za magenge kuwa na mamlaka katika baadhi ya magereza.