NATURAL BEAUTY SECRETS AND TIPS FOR BEAUTIFUL, HEALTHY SKIN(afya , mazoez na urembo)

NATURAL BEAUTY SECRETS AND TIPS FOR BEAUTIFUL, HEALTHY SKIN(afya , mazoez na  urembo)

JOH MAKINI ADAI MUZIKI WA BONGO LAZIMA UBADILIKE, UACHANE NA STAILI HII

Rapper Joh Makini ambae anatesa na kibao chake cha Perfect Comboamedai kuwa vyombo vya habari vikishirikiana na wasanii wa muziki inabidi wabadilishe mfumo uliopo kwa sasa kwenye muziki.
Joh Makini
Joh ameiambia Lindiyetu.com kuwa kwenye tuzo mbalimbali kubwa duniani pamoja na chati za muziki unaweza ukaona msanii mmoja anaingiza nyimbo zaidi ya moja kitu ambacho hapa nchini kimekuwa kigumu kufanyika.
“Nafikiria sisi tukishirikiana na media tukubaliane nahuu wakati kwamba sio wakati wa watu kushangaa kwanini msanii mmoja ana nyimbo tatu kwenye Top 10 au kwanini msanii mmoja anakuwa kwenye category moja mara tatu. Unajua wenzetu kwenye grammy au nchi zilizoendelea hawashangai hili. Nenda Billboard unaweza ukakuta msanii ana nyimbo tano kwenye Top 10, lakini hapa bongo wanasema nyimbo yake namba moja halafu uingize nyingine? ” amesema Joh..
“Hapana huwezi kuweka nyimbo mbili za msanii mmoja kwenye nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu, ni lazima hayo mambo yaishe. Kama kuna mtu anastahili kuwa na nyimbo tano kwenye chati na ni kali inabidi ziwepo kwa sababu hiyo inawafanya watu wengine waingie studio kufanya kazi nzuri zaidi,” ameongeza
Previous
Next Post »