NATURAL BEAUTY SECRETS AND TIPS FOR BEAUTIFUL, HEALTHY SKIN(afya , mazoez na urembo)

NATURAL BEAUTY SECRETS AND TIPS FOR BEAUTIFUL, HEALTHY SKIN(afya , mazoez na  urembo)

Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi

Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi

DESEMBER 30,2016

Obama
Image captionRais wa Marekani,Barrack Obama

Rais Obama wa ameamuru kutimuliwa kwa wanadiplomaisa thelathini na tano wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi kutaka kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.
Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae kuwekewa vikwazo.
Rais Obama amesema Urusi imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani na ametahadharisha hatua zaidi kuchukuliwa.

RUSSIAImage copyrightVIO SWAHILI
Image captionWadukuzi

Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti washtushwe na vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.
Kwa upande wake, rais mteule mara kwa mara amekuwa akizipuuzia taarifa hizo za udukuzi, lakini hivi amesema atakutana na wakuu wa mashushu wa Marekani ili kulijadili hilo.
Urusi nayo imekana tuhuma za kufanya udukuzi mfumo wa mtandao wa chama cha Democratic.
Msemaji wa serikali ya Urusi amesema Urusi nayo italipiza kwa kiwango hicho hicho.
Previous
Next Post »