NATURAL BEAUTY SECRETS AND TIPS FOR BEAUTIFUL, HEALTHY SKIN(afya , mazoez na urembo)

NATURAL BEAUTY SECRETS AND TIPS FOR BEAUTIFUL, HEALTHY SKIN(afya , mazoez na  urembo)

Barafu kubwa kumeguka Antarctica


  • 7  Januari 2017

ice shelf break upImage copyrightADRIAN LUCKMAN
Image captionSiwa barafu hiyo ina ukubwa sawa na robo ya eneo la Wales

Wanasayansi wameambia BBC kuwa barafu kubwa iliyo na ukubwa mara 50 kushinda kisiwa cha Manhattan, Marekani imefikia kiwango cha kupasuka kutoka eneo kubwa la barafu la Larsen C kaskazini mwa Antarctica.
Siwa barafu hiyo inatarajiwa kuwa miongoni mwa 10 kubwa zaidi zilizopasuka kutoka Antarctica.
Mpasuko mkubwa ulionekana kwenye barafu hiyo ghafla mwezi uliopita na kwa sasa ni sehemu ya kilomita 20 za barafu ambayo inazuia kipande hicho kikubwa cha barafu kumeguka na kuelea baharini.
Larsen C ndiyo sehemu kubwa ya barafu iliyo kaskazini zaidi eneo la Antarctica.
Watafiti walisema iwapo eneo hilo litapoteza kipande hicho cha barafu basi sehemu yote yenyewe itakuwa hatarini ya kupasuka tena siku za usoni.
Eneo la barafu la Larsen C lina kina cha mita 350.
Barafu hiyo huelea maeneo ya pembeni Antarctica Magharibi na kuzuia mito ya barafu ambayo huisaidia kukaa imara.
Watafiti wamekuwa wakifuatilia Larsen C baada ya kumeguka kwa sehemu ya barafu ya Larsen A mwaka 1995 na kisha kupasuka ghafla kwa sehemu ya barafu ya Larsen B mwaka 2002.
Wataalamu wanakadiria kwamba iwapo barafu yote kwenye sehemu hiyo ya bahari ya Larsen C itayeyuka na kuwa maji na kuingia baharini, viwango vya maji baharini vitapanda kwa sentimeta 10.

BarafuImage copyrightNASA
Image captionUfa kwenye mpasuko wa sehemu hiyo ya barafu una upana wa 100m lakini una kina cha nusu kilometa
BarafuImage copyrightNASA
Image captionPicha zilizopigwa Novemba mwaka jana zikionyesha ufa uliotokea
Previous
Next Post »